×

Yanayohusu Station 77

Kampuni ya Kiafrika ya utoaji maudhui

Bara liko tayari kubuni Sanaa. Watu wako tayari kutunza. Sasa umefika wakati wa kujumuisha uwezo wa ubunifu.

Sisi ni turubai la kipekee katika ulimwengu wa dijitali ambayo wasanii wabunifu kutoka Kenya pamoja na Afrika yote hutumia kubuni na kutayarisha fikra za kipekee za kuonyesha msukumo kwa dunia yote. Tunaamini katika kuelezea undani wa utamaduni wetu, na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kuboresha uzoefu wa watu kutoka tabaka mbali mbali za kimaisha. Mnapokusanyika pamoja kama wasanii wabunifu mnakuwa kundi moja lenye uwezo zaidi kuliko kuwa kando kando. Mnakuwa kitu kimoja mnapoungana wakati cheche zenu za ubunifu zinapowasha shauku inayoimarika na kufanya kila fikra kuwa maridadi ya kuvutia kwa walimwengu wote kushuhudia.

Tungependa kuwaalika mjiunge nasi, muingie ndani na kubuni kitu maalum kitakacho simama imara na kudumu kwa muda mrefu na kuonyesha ulimwengu wote vitu maridhawa vinavyotoka katika bara hili letu. Twajivunia utofauti wetu na twapenda jinsi tulivyo kwa sababu hiyo ndio utathmini umbo la yote tunayofanya.

Sisi sio tu kundi la wasanii maahiri; sisi ni watayarishi wa fikra na wabuni wa filamu za kipekee. Dhihirisho la umaahiri huu ndio sababu ya kuanzishwa kwa Station 77, na sasa tukiwa hapa tungependa kuwaalikeni nyinyi kujiunga katika harakati hii yetu..

Sisi ni zaidi ya wabunifu. Sisi ni wasanii wabunifu tulioimarishwa na teknolojia ya kileo…

Blogu 77

Blogu yetu inatetea jitihada za ubunifu. Hii ni sauti ya bara hili lote inayokusihi usongee karibu ili usikilize, utazame, ujionee. Tunabuni na tunatunza. Tunaeneza habari, tunavunja mipaka, na tunaunganisha watu. Fuatilia habari kutuhusu na utajionea nini kinachoweza kutoka kwa bara hili letu lilojaa ubunifu tele.

Uwakala wa madhui ni nini?

Kwa mawazo ya kwanza, unaweza kudhania kuwa neno “Wakala wa Maudhui” ni jina lingine tu la “Wakala wa Matangazo”.

Endelea kusoma

Maudhui mazuri ni yapi na yanamaanisha nini kwa chapa yako

Maneno “Maudhui mazuri” yana maana tofuati kwa watu tofauti, lakini kwa undani zaidi yana mafungamano sawa ambayo tunahitaji kuvumbua.

Endelea kusoma

Utunzaji wa maudhui ya kiafrika – Sauti ya utamaduni maarufu kisasa wa Kiafrika

Utunzaji wa maudhui pengine ni wazo ambalo hujawahi kukabiliana nalo. Sio sawa na matangazo au kutayarisha kitu

Endelea kusoma

Ishara Station 77

Royal Comfort,
East Church Road Nairobi, Kenya

+254 722 419 366

jambo@station77.co.ke