×

Yanayohusu Station 77

Bara liko tayari kubuni Sanaa. Watu wako tayari kutunza.
Sasa umefika wakati wa kujumuisha uwezo wa ubunifu.

Sisi ni turubai la kipekee katika ulimwengu wa dijitali ambayo wasanii wabunifu kutoka Kenya pamoja na Afrika yote hutumia kubuni na kutayarisha fikra za kipekee za kuonyesha msukumo kwa dunia yote. Tunaamini katika kuelezea undani wa utamaduni wetu, na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kuboresha uzoefu wa watu kutoka tabaka mbali mbali za kimaisha. Mnapokusanyika pamoja kama wasanii wabunifu mnakuwa kundi moja lenye uwezo zaidi kuliko kuwa kando kando. Mnakuwa kitu kimoja mnapoungana wakati cheche zenu za ubunifu zinapowasha shauku inayoimarika na kufanya kila fikra kuwa maridadi ya kuvutia kwa walimwengu wote kushuhudia.

Tungependa kuwaalika mjiunge nasi, muingie ndani na kubuni kitu maalum kitakacho simama imara na kudumu kwa muda mrefu na kuonyesha ulimwengu wote vitu maridhawa vinavyotoka katika bara hili letu. Twajivunia utofauti wetu na twapenda jinsi tulivyo kwa sababu hiyo ndio utathmini umbo la yote tunayofanya.

Sisi sio tu kundi la wasanii maahiri; sisi ni watayarishi wa fikra na wabuni wa filamu za kipekee. Dhihirisho la umaahiri huu ndio sababu ya kuanzishwa kwa Station 77, na sasa tukiwa hapa tungependa kuwaalikeni nyinyi kujiunga katika harakati hii yetu..

Sisi ni zaidi ya wabunifu. Sisi ni wasanii wabunifu tulioimarishwa na teknolojia ya kileo…